Tuesday, July 24, 2012
ADC YAPATA USAJILI WA KUDUMU
Chama cha siasa cha Allince Democratic Change (ADC), jana wamekabidhi majina ya wadhamini, barua ya maombi na fomu mbalimbali kwenye ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kwa ajili ya kupata usajili wa kudumu wa chama hicho.Akizungumza katika makabidhiano hayo Mwanasheria mwandamizi anayetoka katika ofisi za msajili wa vyama vya siasa nchini Bi. Piencia Etanga ambaye alipokea majina hayo pamoja na fomu za kuomba usajili wa kudumu kama ilivyo kwa mujibu wa sheria.
"Mmetimiza masharti yote mliyopewa ya kutafuta wadhamini ambao wanaotoka Tanzania Bara na Tanzania visiwani ili wawe wadhamini wa kudumu katika chama chenu"alisema Bi.Etanga
Vile vile, alimwambia Katibu Mkuu wa Chama hicho ambaye ni Kadawi Limbu kuwa wakae pamoja na ofisi msajili ili kupanga ratiba ya kutembelea wadhamini sehemu walipo.
"Hatuwezi kutoa cheti cha usajili wa kudumu bila ya sisi wenyewe kuwaona wadhamini waliowadhamini katika chenu na tukisha hakiki tutawapa usajili wa kudumu kwa kuwa masharti na vigezo mtakuwa mmekamilisha vile inavyotakiwa "alisema Bi. Etanga.
Naye,Katibu Mkuu wa Chama hicho Bw. Limbu alisema kuwa wamefatiza masharti kama walivyoambiwa hapo awali walipewa siku 180 kwa ajili ya kutafuta wadhamini na wamefanikiwa.
"Wadhamini waliokuwa wanatakiwa ni kutoka Tanzania bara na Tanzania visiwani ambao wasiopungua 2000 na sasa tumepata wadhamini zaidi ya 3000"alisema Bw. Limbu.
Bw. Limbu alisema kuwa, mikoa waliyopata wadhamini ni Mara, Mwanza, Iringa, Dodoma,Zanzibar Magharibi,Kaskazini Pemba, Mtwara,Lindi, Tanga, Dar es Salaam, na Mjini magharibi.
Chama hicho kilipata usajili wa muda Machi 26 mwaka huu ambapo walipewa masharti ya kutafuta wadhamini wanaotoka Tanzania Bara na Tanzania Visiwani.
Labels:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment