Tuesday, July 24, 2012

RWAKATARE ACHOSHWA NA AHADI ZA SERIKALI


Mbunge wa viti Maalumu Mchungaji Dkt. Getrude Rwakatare (CCM), amedai kuchoshwa na ahadi za serikali ambazo hazitekelezeki . Mchungaji Rwakatare aliyasema hayo bungeni mjini Dodoma jana na kudai kuwa serikali imeshindwa kutoa kipaumbele katika sekta ya miundo mbinu Wilayani Kilombero mkoani Morogoro

Alisema tangu akiwa shule ya msingi barabara ya kilombero imekuwa ya vumbi hadi sasa licha ya serikali kutoa ahadi ya kujenga bila ya mafanikio

“Wilaya hii ni ya muda mrefu lakini haipewi kipaumbele kwa kiwango cha lami, jambo hili linasikitisha “ alisema

Awali katika swala la msingi Mchungaji aliitaka serikali ieleze ni lini ujenzi wa barabara ya lami kutoka Kidatu Taveta utaanza kutelekezwa

Akijibu swali hilo Naibu wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge alisema ujenzi wa barabara ya kidatu ifakara Taveta umekuwa ukitekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha alisema ujenzi wa kilometa 10 za lami kutoka Kiberege Magereza hadi Ziginali, ulikamilika mwaka 2006 na ujenzi wa kilometa 6.17 za lami kutoka Kibaoni Ifakara, miji iliyokamilika mwaka 2008

No comments:

Post a Comment