Tuesday, June 19, 2012

WASANII WAJENGEWA NYUMBA

Wasanii  mbalimbali nchini wanatarajia kujengewa nyumba zaidi ya 200 katika mradi endelevu eneo la Mkulanga Mkoa wa Pwani kupitia chama chao.
Hayo yalisemwa Dar es Salaam juzi na Mwenyekiti wa SHIWATA Tanzania Cassim Taalib katika Kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na televisheni ya TBC One.

Taalib alisema kuwa mpango huo wa ujenzi wa nyumba hizo unatarajia kukamilika mda mfupi kutokana na kuweka mikakati kabambe na wasanii nchini.

"Kwa sasa ujenzi wa nyumba tano umekamilika eneo la Mkulanga ikiwa ni matunda ya chama hicho kwa kazi zilizofanywa na wasanii wetu kuifadhi kipato chao"alisema Taalib.

Alisema kuwa mikakati ya chama hicho walivyojiwekea kila mwanachama anayejiunga ndani ya chama anatakiwa kutoa shilingi 200,000 kila baada miezi mitano ambapo fedha hizo ndio zinatumika kujengea nyumba hizo..

Taalib alisema kuwa kwa sasa wameweza kuwekeza ukubwa ekali 500 za shamba mali ya wasanii nchini kama kitega uchumi chao kiweze kuja wasaidia.

Malengo ya baadae ni kujenga hoteli na uwanja mpira kwa ajili ya kuongeza kipato cha wasanii na jumla ya wasanii waliokuwepo mpaka sasa ni 5000.

Pia alisema kuwa kwa mwanachama mpya ambaye atapenda kujiunga aweze kuwa mwanachama halali fomu shilingi 8000 na baadae anatakiwa atoe shilingi 200,000 kwa ajili ya kutunisha mfuko na sababu kuu ya kubuni mbinu hiyo wasanii kukosa msada wa kusaidiwa katika shuguli zao.

No comments:

Post a Comment