Tuesday, June 19, 2012
SERA NDIO KIKWAZO KWA MKULIMA NCHINI
Sera pamoja na mfumo wa serikali ndio kikwazo cha kumkandamiza mkulima, mfanyabiashara mdogo pamoja na mlaji katika masoko ya kikanda ya Afrika mashariki pamoja na jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika(SADC)
Akizungumza katika warsha iliyo andaliwa na banki ya dunia kwa ajili ya kukuza biashara ya kikanda katika mazao ya chakula na jukumu la kimkakati la viwango Bw Josaphat Kweka, ambaye ni mchumi mwandamizi wa kupunguza umasikini alisema, inabidi kuangalia sera na kuwa na sera bora ambazo zenye msimamo wa kumuwezesha zaidi mkulima kuliko kumkwamisha
Alisema ukizungumzia sera unazungumzia taasisi za viwango, ambazo nchi kwetu ziko tano na zote zinashungurika na maswala ya viwango na kwa misingi mbalimbali ya kisheria
Alisema kuwa taasisi hizo mara nyingi zinaonekana kuwa ni tatizo kwa yule ambaye anatakiwa kufaidika na vile viwango hivyo inasababisha ugumu kwa mkulima kulifikia soko la kanda pamoja na ushindani wa biashara
Bw. Kweka aliongezea kwamba taasisi hizo zibadilishiwe mfumo wa kisera ili kwamba asasi za viwango ziwe za kuwezesha zaidi na badala ya kukwamisha ili kuweza kupata ushindani wa masoko ili kumuwezesha mkulima, mfanyabiashara pamoja na mlaji mdogo waweze kunufaika
Aliongezea kuwa katika swala zima la biashara ya kimataifa na ushirikiano wa kikanda inamsaidia mkulima mdogo aweze kufaidika zaidi na suala la kilimo na badala ya kukwamishwa
Labels:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment