Wabunge wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Simba na Yanga wanatarajia kucheza mechi ya
aina yake Julai 7 mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Lengo la mechi hiyo ni kuwakutanisha watanzania kuwa kitu
kimoja pamoja na kuchangia mfuko wa elimu kwa asilimia 20 ya mapato
yatakayopatikana siku hiyo.
Akizungumza na mwandishi wa habari jana jijini dar es Salaam
Mratibu wa mechi hiyo Juma Mbizo ambaye pia ni mkurugenzi wa ukumbi wa Dar Live alisema, wameamua kufanya tamasha
hilo ili kuisaidia serikali kujenga
mabweni ya shule kwa upande wa wasichana hapa nchini.
"Tamasha hilo litakuwa la aina yake hasa pale
tutakapowaona waheshimiwa wakichuana kwa lengo la kubadilishana mawazo ya nchi
kujua wapi walipo na tunapokwenda,"Alisema Mbizo.
Aliwataka wadau mbali mbali wa soka kujitokeza kwa wingi
siku hiyo kushuhudia viwango vitakavyoonyeshwa na wabunge hao badala ya kusikia kupitia vyombo vya habari
Pamoja na hayo kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka Bongo Muvi na Bongo Fleva wakiwemo wasanii wa kizazi kipya pamoja na Chameleon wa Uganda vile vile kutakuwa na pambano la ngumi ambalo litawakutanisha mabondia Cheka na
Kaseba
No comments:
Post a Comment