Thursday, June 21, 2012

VODACOM YAINGIA UBIA NA TAN TRADE

Kampuni ya Simu za mkononi ya Vodacom Tanzania imeingia ubia na mamlaka ya maendeleo nas Biashara Tanzania (TanTrade) kuwa mdhamini wa sekta ya mawasiliano katika maonyesho ya kimataifa ya biashara Sabasabasa yanayofanyika kila mwaka jijini Dar es salaam.

Akizungumza Dar es salaam jana katika mkutano na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza alisema Vodacom Tanzania itaendesha matangazo yote kuhusiana na ushiriki wa maonyesho  hayo ya sabasaba ambayo yanatarajia kuaza Juni 30 mwaka huu katika viwanjwa vya maonyesho vya mwalimu Julius Nyerere.

"Ushirikiano huu umekuja ambapo sekta ya mawasiliano imekuja na changamoto tangu mfumo wa kimaisha ya kijamii kubadilika ambapo watanzania wengi wanatumia huduma ya simu kama njia ya kubadilishana mawazo katika ngazi ya familia na shughuli za kiofisi"alisema

"Tumegundua hili na ndiyo maana takaleta huduma ya kuamisha fedha ya Vodacom M-pesa hivi sasa huduma hii imekuwa ni msingi kwa watanzania walio wengi "alibainisha Bw. Meza.

Aliongeza kuwa Vodacom Tanzania itaendelea kutoa huduma bidhaa ambazo ni rahisi na nafuu kwa wateja wote nchini na kuweza kufurahia.

Alisema Vodacom Tanzania imewekeza kwa kiasi kikubwa katika maendeleo na maboresho ya miundombinu kupitia kampuni hiyom inatarajia kuboresha ubora wa huduma na bihaa zinazotolewa kwa wateja ambapo sasa wataweza kumudu gharama za huduma na bidhaa hasa kwa vijana ili kuongeza watumiaji wa huduma hiyo.

Maonyosho ya kimataifa ya sabasaba yanayofanyika Dar es salaam kila mwaka ni maonyesho ya kibiashara yanaongoza Tanzania ambapo yanavutia wageni zaidi 3,50,000 na kujenga mahusino na maingiliano baina ya watoa huduma na wateja wao ikiwa pamoja na kulinganisha ubora wa bidhaa katika kila nchi washiriki.






No comments:

Post a Comment