Thursday, June 21, 2012
KAMPUNI 430 KUSHIRIKI MAONYESHO SABASABA
Zaidi ya kampuni 430 ya kigeni na Mataifa 11 yanatarajia kushiriki maonyesho ya 36 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayotarajiwa kuanza Juni 28 ambapo tarehe 1 Julai yatafungulia rasmi kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere vilivyopo Barabara ya Kilwa.
Hayo yalisemwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya biashara (TanTrade) Bw.Samwel Mvingira alipokuwa akizungumza na Wandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.
"Makampuni 435 na nchi 11 pamoja na washiriki wa ndani 1500 wanatarajiwakushiriki maonyesho ya mwaka huu "alisema Bw.Mvingira.
Awali Bw.Mvingira alisema sambasamba na ufunguzi huo kutakuwa na zoezi la kushindanisha vibanda ambalo linaanza tarehe 28na kumaliza 30 Julai ambapo mgeni rasmi atamtangaza mshindi.
Wakati huohuo Bw.Mvingira aliongezea kwa kusema nchi ya Rwanda na China ndio washiriki pekee walioleta wanachama wengi kuliko nchi zengine ambapo Rwanda peke yake wamechukua eneo la mita za mraba 400.
Sambasamba na hilo alikanusha kauli za baadhi ya wafanyabiashara wadogo wadogo waliolalamika kuhusu sabasaba hall kupewa wachina.
Bw.Mvingira alisema SabaSaba hall na Karume hall yameandaliwa kwa washiriki kutoka nje kwa sababu ya gharama ya eneo hilo kuwa kubwa ambapo mfanyabiashara wa kawaida hawezi kumudu.
"SabaSaba hall na Karuma hall yanakodishwa kwa eneo la mita ya mraba 1 na sawa na Dola 150 na banda linachukua karibu eneo la mraba mita 9 kwaiyo gharama yake ni kubwa,wafanyabiashara wa kawaida watakuwa Mwinyi hall na Mkapa hall"alisema Bw.Mvingira.
Kwa upande wa viingilio katika maonesho hayo itakuwa wakubwa sh.2,500,watoto 500 kwa siku za kawaida.Wakati wa kilele cha mahadhimisho hayo Julai 7 mwaka huu kingilio cha wakubwa kitakuwa sh.3,000 na watoto sh.1000.
Hata hivyo ametoa wito kwa washiriki kufuata sheria kwa kipindi chote cha maonesho ambayo yanatarajiwa kufungwa rasmi julai 8.
Labels:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment