Hiki ni kijitabu kidogo ambacho kimetayarishwa na Deus Kibamba, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo
cha Taarifa kwa Wananchi (TCIB) na Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania kwa kushirikiana na Hebron Mwakagenda na Kuhaririwa na Profesa Chris Peter Maina, Mhadhiri Mwandamizi katika Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Madhumuni ya kitabu hiki ni kujenga na kuongeza uelewa wa watanzania juu ya Katiba, historia yake na mchakato wa uandikaji wa Katiba hapa nchini na duniani. Dhumuni la pili ni kuwatoa hofu watanzania kuwa uandikaji wa Katiba si suala la wanasheria tu bali ni kazi inayotakiwa kufanywa na wananchi wote. Jambo kubwa ni uelewa wa namna wananchi wanavyoweza kushiriki.
soma kitabu hiki ujielimishe,
Hii ni habari njema kwa raia wengi wa nchi hii ambao hawajawahi kupata fursa ya kuisomakatiba ya nchi yao
ReplyDelete