Wednesday, June 20, 2012

FILAMU YA UKATILI YAWALIZA MABALOZI



Mabalozi na Wanadiplomasia wa nchi mbalimbali, wamesikitishwa na filamu ya Ukatili dhidi ya Watoto, iliyoonyeshwa kwa muda wa dakika tano kwenye Ukumbi wa Serena jijini Dar es Salaam . Filamu hiyo ilionyeshwa juzi katika mdahalo wa Ukatili dhidi ya watoto kwa wadau mbalimbali ili kuonyesha Tanzania inavyopambana na ukatili dhidi ya watoto baada ya ripoti ya ukatili dhidi ya watoto kuzinduliwa mwaka jana


Mgeni rasmi katika mdaharo huo alikuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya jamii Jinsia na Watoto , Ummy Mwalimu, ambaye alisema filamu hiyo inaonyesha ni jinsi gani Tanzania inathamini haki za watoto

Alisema kuwa serikali imeweka wigo mpana katika kutetea haki za watoto na filamu hiyo imeonyesha ni jinsi gani inatoa uhuru kujadiliwa kwa haki za watoto katika midaharo mbalimbali

Aidha filamu hiyo pia ilitazamwa na Mkuu wa Jeshi la polisi nchini, Said Mwema ambaye kwa upande wake alisema kuwa jeshi lake linapambana na vitendo vya ukatili kwa watoto kwa kuanzisha madawati mbalimbali ya watoto katika vituo vya polisi

No comments:

Post a Comment