Thursday, August 2, 2012

WAASI WALAANIWA KW MAUAJI SYRIA




Wapiganaji wa kundi la waasi nchini Syria wamelaaniwa vikali baada ya picha moja ya video iliyowekwa kwenye mtandao wa internet kuwaonyesha wakiwauwa kwa kuwapiga risasi wanaume kadhaa walioshutumiwa kuwa wanamgambo wanaoiunga mkono serikali.

Waasi wakiwazuilia wanamgambo wanaoiunga mkono serikali

Shirika la kutetea haki za binadamu, Human Rights Watch, picha hiyo, ambapo wanaume hao wanawekwa ukutani na kisha kumiminiwa risasi-huenda inaonyesha vitendo vya uhalifu wa kivita.

Picha za kutisha zimewaonyesha waasi wenye silaha wakiwaua kikatili watu wanaoaminika kuiunga mkono serikali ya Rais assasd katika mji wa Aleppo.

Video hiyo iliyorekodiwa na wanaharakati inaonyesha zaidi ya mateka kumi na wawili waliotambuliwa kama wafuasi wa kundi la wapiganaji la Shabbiha wanaounga mkono serikali.

Wanadaiwa kuwaua wapiganaji kumi na watano wa kundi la waasi la Free Syrian army katika siku za hivi karibuni.

Video hiyo inaonyesha kiongozi wa waasi na wafuasi wake kadhaa wakipelekwa katika eneo na kundi la wapiganaji wenye silaha waliokuwa wakishangilia.

Wanapelekwa hadi karibu na ukuta na kisha wanapigwa risasi na miili yao kuwekwa pamoja. Kumekuwepo ripoti za wapiganaji kutekeleza vitendo vya unyanyasaji lakini vitendo hivyo havijawahi kurekodiwa.

Ni wazi kuwa waasi wanadhibiti maeneo kadhaa ya mji wa Aleppo na kuendelea katika maeneo mengine. Kuna ripoti kuwa huenda wamepata msaada wa silaha zenye uwezo wa kudhibiti mashambulio ya serikali.

Wanaharakati wanasema majeshi ya serikali yamewaua watu wengi katika mapigano ya hivi karibuni katika vitongoji vya mji mkuu Damascus.

Baraza la kitaifa la upinzani nchini Syria limeshtumu waasi hao wenye silaha kwa kuwaua wafungwa wanao unga mkono sererikali katika mji wa Aleppo. Shirika la kutetea haki za binadam la human rights watch limesema video hiyo inaonyesha vitendo vya uhalifu wa kivita.
 
source: bbc swahili

No comments:

Post a Comment