Moja ya kazi ya gwaride la Mashoga , ni kuutaka uma uwakubali kuwa nao wanahaki na jamii isiwaone tofauti. Na nia nyingine inatazamwa kuwa ni kama kupata mda wa kujumuika pamoja na makundi yanayowa unga mkono.
Mmoja wa mashoga hao alisikika akilalamika " kwa nini watu wanatuchukia, kwa sababu sie tunachokifanya ni kuoneshana mapenzi kwa sisi wenyewe na sio kama tunafanya mambo yetu hadharani!!. nasi tuna uhuru wa kufanya vile tunajisikia, kupigana kisi tunaweza fanya barabarani hiyo inakubalika"
Wanachokifanya kipo ndani ya haki za Binadamu; Swali la kujiuliza kama yanayofanyika ni sawa na pengine binadamu anaendelea kuelekea wapi?..haya ni maendeleo au la!!
Hivi karibuni pamekuwepo na mashinikizo kutoka mataifa yaliyoendelea kuwa nchi za Afrika zinapaswa kukubali ndoa ya jinsia moja.Hii ni changamoto kubwa kwa nchi hususani za Kiafrika ambazo tamaduni zao haziruhusu ndoa ya jinsia moja.
Kanisa Katoliki pamoja na Islam, hazikubali Ushoga.
Pia kwa nyakati tofauti baadhi ya watu mbalimbali wamehusisha jambo hili na enzi za sodoma na gomora(Bible) ambapo watu walizidi kufanya uasherati na Mungu akaja kuwateketeza.
Toa maoni yako.
No comments:
Post a Comment