Saturday, July 21, 2012
MTOTO ALIYEPOOZA ARUDI NCHINI
Mtoto Imran Mwerangi (3) aliyepooza mwili baada ya kuchomwa sindano amerudi kutoka nchini India alikoenda kwa ajili ya matibabu ingawa hali yake bado haijatengamaa
Akizungumza na mwandishi mama mzazi wa mtoto huyo Bi. Amina Machulo alisema kuwa kwa sasa mtoto huyo anaendelea vizuri ingawa hajapona kabisa kwani bado hawezi kutembea wala kuongea kama awali kabla hajapata tatizo hilo
“Tunamshukuru mungu amepata nafuu ingawa hawezi kutembea kama awali,kucheza na wenzake kama tulivyozoea kumuona kula amekuwa ni mtu wa kitandani muda wote” alisema
Mama huyo alisema kuwa kila baada ya miezi sita wanatakiwa kurudi nchini India kwa ajili ya kuendelea na matibabu na kuhakikisha afya yake inazidi kuimarika, ingawa garama za kwenda nchini humo zinagaramiwa na serikali
Aliongezea kuwa Madaktari wameshauri mtoto aendelee kutumia dawa pamoja na kupata chakula bora na kuendelea na mazoezi ili kujalibu kufanya uponyaji wake uwe wa haraka na kurudi katika hali yake ya mwanzo
Mtoto huyo ambaye alikuwa anasumbuliwa na tatizo la nyama za puwa na baada ya kuchomwa sindano ya usingizi inasemekana kuwa ndio iliyomletea tatizo la utindio wa ubongo na kusababisha kupooza mwili
Alilazwa katika hospitari ya taifa Muhimbili(MNH)katika chumba cha wagonjwa mahututi takribani miezi 7 kabla ya kupelekwa nchini India kwenye matibabu zaidi
Labels:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment