Tuesday, July 31, 2012

MMAREKANI AKIRI KUFANYA NJAMA KUISAIDIA KUNDI AL-SHABAB


                                                      Wapiganaji wa al-Shabab
Mmarekani aliyetuhumiwa kwa kujaribu kujiunga na kundi lenye msimamo mkali la Kiislam la al-Shabab nchini Somalia amekiri mashtaka yake kwenye mahakama Marekani.

Shaker Masri, 28, alikamatwa Agosti 2010 akijiandaa kusafiri kwenda Somalia kukijunga na al-Shabab, kwa mujibu wa mwendesha mashtaka wa Marekani.

Marekani na Uingereza wanaliona kundi hilo likijihusisha na al-Qaeda, kuwa ni kundi la kigaidi.

Katika makubaliano ya kukubali mashtaka, Masri amekubali kutumikia kifungo chini ya miaka kumi gerezani.

Alikiri kupanga njama za kukusanya fedha alizohitaji kujzitumia katika jihadi ama Somalia au Afghanistan.

Amehukumiwa kifungo za miaka 15 gerezani.

Masri alizaliwa Alabama na kuishi Chicago kabla ya kukamatwa saa chache hajaondoka nchini.

Amekuwa akijieleza kama wakala wa FBI wa siri na amekuwa akizungumzia kuhusu kuwalenga ‘makafiri’

Kufuatia kukamatwa kwake alishtakiwa kwa kujaribu kusaidia kwa mali kundi la kigaidi, akijaribu kuwapa msaada kwa kutumia silaha za maangamizi.

Taarifa kamili za kukiri kwake hazijatolewa kwa umma.

Al-Shabab wanaamini kuwa ikiwapata wasomali wenye asili ya Kimarekani kushiriki katika kujitoa muhanga nchini Somalia na maafisa wa Marekani sasa wana wasiwasi wa kuwepo shambulio ndani ya Marekani.

Raia kadhaa wa Marekani wamekamatwa katika miaka ya karibuni wakijaribu kushiriki au kuunga mkono vita vya zaidi ya miongo miwili iliyopita.

Shaker Masri atahukumiwa rasmi mwezi Oktoba 16.
source:bbc swahili

No comments:

Post a Comment