Tuesday, July 31, 2012

MCHINA MSHINDI KUOGELEA- HAJATUMIA DAWA



Msichana muogeleaji wa China Ye Shiwen hajatumia dawa kwenye michezo, mwenyekiti wa Kamati ya Olympiki Uingereza. Amesema hayo baada ya kocha wa Marekani kuonyesha wasiwasi wa kuvunja kwake rekodi ya dunia katika mshindano ya kuogelea.

Mwenyekiti huyo Lord Colin Moynihan amesema Ye, mwenye umri wa miaka 16, alipitia hatua zote za kupimwa kama anatumia dawa hizo na kukutwa kuwa ni safi na anastahili kutambuliwa kwa kipaji chake.

Ye alivunja rekodi yake mwenyewe kwa sekunde tano katika mita 400 Medley.

Kocha mwandamizi wa Marekani John Leonard alisema kufanikiwa kwa binti huyo kulikuwa na mashaka huenda kulikuwa udanganyifu wa kutumia dawa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la makocha wa mchezo wa kuogelea Bw Leonard amesema kufanikiwa kwa mwanamichezo huyo wa China kunamkumbusha mashindano ya kuogelea kwa wanawake ya miaka ya 1980 Ujerumani Mashariki waliokuwa wakitumia utaratibu wa udanganyifu.

"Historia katika mchezo wetu itakuwambia kuwa kila mara tukiona kitu na nitaweka kwenye nukuu kuwa, ‘si rahisi kuamini, historia inaonyesha inageuka baadaye kuwa udanganyifu ulihishwa,"aliliambia gazeti la Guardian la Uingereza.

Lakini Ye, ambaye baadaye atamalizia mashindano ya fainali ya mita 200,amejitetea mwenyewe kwa nguvu na kukana kuwa hajawahi kutumia dawa zozote.

Mkuu wa kuzuia udanyanyifu wa dawa kwenye michezo nchini China amesema binti huyo amefanyiwa uchunguzi mara zaidi ya mia moja tangu alipofika London na hakuna kipimo hata kimoja kinachoonyesha kuwa alikuwa ametumia dawa.

Waogeleaji wa zamani na washindi wengine wa Olympiki na hata waatalam wamekuwa wakimuunga mkono Ye.

Lord Moynihan ameviambia vyombo vya habari kuwa kitengo cha kupambana na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu kinadhibiti vilivyo suala hilo kwenye michezo hii ya Olympic

"Amepitia kwenye mpango wa Wada kwa hiyo yuko safi. Huu ndio mwisho wa habair hii. Ye Shiwen anastahili kwa kipaji chake." Alisema.

Mwenyekiti wa Kamati ya Olympic Marekani (USOC) amejitenga na maoni ya Bw Leonard na Patrick Sandusky, msemaji wa kamati ya Marekani ameiambia BBC kuwa Wamarekani wanajaribu kumaliza mambo haya na China kwa utaratibu mzuri.

Mmoja wa wajumbe wa wa timu ya uhusiano wa kimataifa ya USOC anatarajiwa kukutana na kamati ya Olympic ya China baadaye Jumanne, kwa mujibu wa mwandishi wa BBC David Bond.

source:bbc swahili

No comments:

Post a Comment