Mkuu wa chuo kikuu cha Tiba (KCMC), cha mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, Prof.
Egbert Kessy, amesema kuwa kuwepo kwa vazi la Taifa kutasaidia kuitambulisha
Tanzania.
Prof. Kessy aliyasema hayo juzi wakati wa hafla ya kufunga tamasha la utamaduni wa mwafrika, lililofanyika chuoni hapo na kuwashirikisha wanafunzi kutoka nchi kadhaa za Afrika na wale wa Kitanzania wanaosoma chuoni hapo.
Prof. Kessy aliyasema hayo juzi wakati wa hafla ya kufunga tamasha la utamaduni wa mwafrika, lililofanyika chuoni hapo na kuwashirikisha wanafunzi kutoka nchi kadhaa za Afrika na wale wa Kitanzania wanaosoma chuoni hapo.
“Utandawazi umechangia mambo mengi ya kimaendeleo lakini kwa upande mwingine umechangia pia kumomonyoka kwa maadili ya mwafrika haswa kwa upande wa vijana ikiwemo kwenye mavazi”, alisema
Alisema vazi la Taifa litakuwa mchango mkubwa katika kuitangaza Tanzania sanjari na mambo mengine ambayo yamekuwa yakiitambulisha Tanzania duniani kote.
Prof. Kessy aliendelea kusema kuwa kuna mambo mengi ambayo Watanzania wamekuwa wakitofautiana kwenye baadhi ya masuala kama wanajamii wengine ambapo alisema tofauti hizo zitamezwa na uwepo wa vazi la Taifa ambalo alisema litakuwa ni kiunganishi cha Watanzania wote bila kujali aina ya itikadi wanazozifuata.
Aidha alitoa wito kwa wasomi nchini kote kuihamasisha jamii katika kipindi hiki ambacho mchakato wa kutafuta vazi la Taifa ukiendelea, ili Watanzania waone umuhimu wa kushiriki katika mchakato huo jambo ambalo alisema litachagia kupatikana kwa vazi hilo.
No comments:
Post a Comment