UONGOZI wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), umewarejesha kazini baadhi ya madaktari walioondolewa hospitalini hapo baada ya kubainika hawajashiriki katika mgomo.
Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi wa Utumishi MNH, Bw. Makwai Makani, ilisema madaktari hao ni wale waliokuwa wakifanyakazi kwa vitendo.
Alisema madaktari 20 wa Idara ya Maabara, 45 Idara ya Famasia wanatakiwa kuripoti kazini haraka na kuwataka madaktari sita waliokuwa likizo, kurejea kazini na pamoja na wengine 41.
Wakati uongozi wa hospitali hiyo ukifikia hatua hiyo, haijafahamika kama Madaktari Bingwa ambao waliamua kutangaza mgomo kama watarejea kazini wakidai kuwa, hawawezi kufanyakazi bila kuwa na wasaidizi wao.
Wakati huo huo, huduma za matibabu kwenye Taasisi ya Tiba na Mifupa (MOI), jana ilianza kuimarika baada ya wagonjwa kuanza kupata huduma.
No comments:
Post a Comment