Tuesday, June 26, 2012

LEMA AWAUNGA MKONO MADAKTARI



Uongozi wa Hospitali ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI), Muhimbili umekiri kuwepo kwa mgomo wa madaktari ambao umeathiri utendaji wa kazi katika kitengo hicho hali inayopelekea kutoa huduma kwa wagonjwa wa dharula tu


Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Ofisa uhusiano wa kitengo hicho Bw. Almas Jumaa alisema kutokana na kuwepo kwa mgomo huo baadhi ya huduma katika kitengo hicho zimesitishwa.

"Mgomo huo umeathiri utendaji wa kazi na sasa wagonjwa wanaopokelewa ni wale wa dharula tu na wanatibiwa na madaktari bingwa, " alisema.

Alisema hivi sasa huduma za wagonjwa watu binafsi hazitolewi kulingana na uhaba wa madaktari.

Aliongezea kuwa madaktari ambao ni viongozi  ndio wanaofanyakazi ya kuzunguka wodini tofauti na awali ambapo kazi hiyo ilikuwa ikifanywa na madaktari wa ngazi zingine.

Pamoja na hayo katika  Hospitali  ya Mwananyamala pamoja na Amana mgomo unaendelea katika  hospitali hiyo kutokana na madaktari hao kutoonekana kama ilivyokawaida.

Katika Hospitali ya Temeke hali ilikuwa tofauti na hospitali zingine kutokana na madaktari hao kuendelea na huduma kama kawaida.

Hata hivyo aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini CHADEMA,Bw.Godbles Lema,alisema ili Serikali kuondokana na kero hiyo ni bora wakachukua sh. bilioni 300 ambazo zinadaiwa kukutwa katika akaunti sita tofauti za Watanzania wakiwamo wanasiasa kwenye benki mbalimbali nchini Uswisi.

ALisema fedha hizo zitakuwa zimeingizwa kiufisadi hivyo ni bora zikachukuliwa na kuwalipa madaktari na walimu ili kumaliza migogoro inayoendelea.

Akizungumza na waandishi katika Hospitali ya Muhimbili, Bw.Lema alisema anakubaliana na uamuzi wa madaktari kugoma kwa kuwa madai wanayodai ni haki yao ya msingi.

Hata hivyo Bw.Lema alisema anaunga mkono mgomo huo kwani mfumo wa nchi yetu unawakandamiza baadhi ya watu.

"Huwezi kupata haki yako bila ya kudai na kuwepo kwa misuguano hivyo kutokana na mgomo huo baadhi ya wagonjwa najua watapata shida lakini naomba tufahamu hilo, " alisema.

Baadhi ya wananchi waliohojiwa na gazeti hili wamewaomba madaktari hao kusitisha mgomo huo kwani wanaoathirika zaidi ni wananchi na hasa wa hali ya nchi

No comments:

Post a Comment