Tuesday, June 19, 2012

DAWA BANDIA NI TATIZO DUNIANI

MAMLAKA ya Chakula na Dawa Tanzania TFDA imesema kuwa suala la dawa bandia ni tatizo la Dunia nzima hivyo amewataka wananchi kushirikiana na Serikali kuziba mianya ya uingizaji dawa bandia ili kulinda maisha ya watanzania kwa ujumla
.

Hayo yalisemwa Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi wa TFDA Bw.Hiti Silo katika viwanja vya Karimjee.wakati wa kufunga madhimisho ya siku ya famasia nchini.

Bw.Silo alisema kuwa kutokana na tatizo hilo kuwa la kidunia hivyo akuna budi kwa wadau,taasisi wananchi kushirikiana na mamlaka hiyo pamoja na serikali kudhibiti njia za uingizaji wa bidhaa bandia.

"Kutokana na changamoto hizi TFDA imeweza kuunda vikosi kazi kwa ajili ya kusimamia udhibiti wa dawa bandia kila pembe ya nchi kwa kushirikiana na jeshi la Polisi kulinda mifumo ya njia hizo"ali
sema Bw.Silo.

Aliwaomba wananchi wanapopata taarifa za uingizaji wa dawa bandia kutoa taarifa ngazi zinazohusika ili wahusika waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Alisema kuwa mamlaka hiyo pia imeweza kuimalisha mipaka yote katika vituo vya forodha zinapoingia bidhaa kwa ajili ya ukaguzi kabla mzigo kurusiwa kuingia nchini.

Kwa upande wake Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt.Hussein Mwinyi alikabidhi cheti kwa Mamlaka ya chakula na Dawa Tanzania TFDA na taasisi zingine zilizoshiriki madhimisho hayo ya siku ya famasia na kuwataka kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi ili wajuwe matumizi ya dawa bandia.

No comments:

Post a Comment