Saturday, November 17, 2012

ISRAELI YAIPIGA GAZA NA MAKOMBORA

Mlipuko mkubwa Gaza
Kutoka ukanda wa Gaza - Israeli imeipiga kwa makombora  takribani mia mbili katika mji wa Gaza. masahmbulizi hayo amabayo yamefanyika Punde leo hii jumamosi, ni kama kulipiza kisasi kwa kundi la Hamasi ambalo lilituma makombora yake kueleke mji Mtakatifu wa Jerusalem (THE HOLLY LAND). Mashambulizi hayo yamesemekana kuuwa watu takribani kumi yaliyokuwa yame elekezwa  kwenye jengo Waziri Mkuu wa Palestina, Kituo cha polisi, na office za mitandao ya internet.



Vikosi zaidi vya majeshi ya Israeli vimezidi kumiminika upande wa mpaka wa Gaza, na masambulizi ya makombora ya kivita kuelekea gaza yakifanywa kwa kutumia nguvu kidogo. Hii inatokana na tukio Hamas la kujaribu kuipiga JERUSALEM.



Israeli katika kukabiliana na mashambulizi hayo, imeibua kifaa chake cha kivita ambacho kimetengeneza yapata miezi miwili iliyopita kwa ajili ya kujikinga na makombora ya maadui zake endapo watapanga kuipiga Israeli haswa katika Mji wa Jerusalem ambao ndio chanzo kikubwa cha Ugomvi kati ya nchi za Kiarabu na Israeli.

Israeli imetishia kuendelea kupanua wigo wa vita endapo makombora ya kundi la Hamas hayatasitishwa.


soma zaidi:  http://news.yahoo.com/israel-launches-scores-airstrikes-gaza-092137360.html

No comments:

Post a Comment