Monday, July 23, 2012

WAKINADADA NA MAVAZI YA MTEGO


Hivi sasa imekuwa kawaida baadhi ya kina dada kila shughuri hasa za usiku kukuta wamevaa nguo fupi, wengi wanasema wanaenda na wakati, vyema, lakini kinachojitokeza zaidi ni tabia ya wadada hawa kutokupenda kuvaa chochote ndani pamoja na kuwa wanavaa nguo fupi, kutokuvaa nguo ya ndani si tatizo sana, lakini je ni lazima watu wajue kuwa hukuvaa kitu??


Wengi wanahusisha ama kuwa na tafsiri tofauti juu ya matendo haya,Wapo wanaodhani ni kwenda na wakati ama mitindo, wapo wanaodhani kuwa huu ni ufuska, lakini pia wapo wanaosema kuwa kila mtu ana haki na kile apendacho kuvaa kwa wakati hautakao muhusika.

 Lakini kuna baadhi ya wadau wana mawazo tofauti kabisa, wao wanadai kuwa moja ya sababu ya tabia hii kushika kasi ni tabia ya kina baba kujifanya hawaoni ama wako bize sana, hawa wanadai kuwa pengine ni kutokana na kina dada kuwa wengi ama kina kaka kuchelewa kuoa, hivyo kina dada wanatafuta mbinu ya kuwashtua ili wajue kuwa nao wapo, sina hakika lipi ni lipi, pengine weye waweza nisaidia katika hili.

Zipo sababu nyingi zinazoweza kusababisha kina baba/kaka kutowaona kina-dada ama kuwaona sawa na wao, baadhi yaweza kuwa ni kupoteza hamu ya kuwa na mwenza kutokana na ama msongo wa mawazo au miangaiko ya maisha, lakini pia iko sababu inayohusisha staili ya maisha na vyakula tulavyo vinachangia kwa kiasi kikubwa kutojisikia kushiriki na mwenzi wako ama kuwaona mabinti kama makaka,


No comments:

Post a Comment