Tuesday, July 24, 2012
UTAMADUNI UWE NDANI YA KATIBA MPYA
Utamaduni unatakiwa uingizwe katika mchakato wa katiba mpya na wasanii wapate nafasi ya kutoa maoni wao na jinsi ya kuulinda utamaduni huo kwani ndio utambulisho wa taifa letu
Hayo yalisemwa na muimbaji wa muziki wa bendi ya Kilimanjaro, John Kitime wakati akizungumzia swala la wasanii kushindwa kufika katika ngazi ya kimataifa alisema kuwa utamaduni lazima uwepo katika katiba mpya kwani nchini kwetu kuna makabila mbalimbali zikiwemo lunga , nyimbo lazima ziwepo kwani ndivyo vitu vinavyozalisha utamaduni wa nchi
Alisema kuwa kwa kuyalinda makabili yetu pamoja na lugha zetu si kwa nia ya kuendeleza ukabila bali ni kuendeleza utamaduni wetu pamoja na kuwafundisha wanachi kuona na kuthamini utamaduni wake ndio mzuri kuliko ule wa mwenzie
“Kwa kutokuthamini utamaduni wetu vijana wanaiga wakiona wenzao wameshusha suruali wao wanavua yakwao inasikitisha kwani kuna watu wakisikia Obama anakuja kutawala nchi wataingia mtaani na kufurahia hii inasababishwa na kutojua thamani ya utamaduni wetu” alisema Kitime
Pamoja na hayo Kitime alisema kuwa wasanii wengi wanashindwa kupeleka kazi zao katika ngazi ya kimataifa kwa kutokuwa wabunifu wa kazi zao na kujivuni mashahiri
Aliongezea kuwa kunatatizo katika mfumo mzima kwani msanii anataka kutoka ikimaanisha kuwa wanataka kupata kipato na kukuza jina ndani ya nchi, na wasambazaji wa kazi zao ni wahindi ambao nao wanaangalia soko na faida hivyo wanasaidia katika kazi zinazo uza na si kwa lengo la kupeleka kazi kimataifa
Alisisitiza kuwa watangazaji nao ni sifuri kwani hawana elimu yoyote kuhusu muziki na pia hawataki kujifunza wanatumia ujanjaujanja kwani hawajui muziki ulipotoka, hivyo mfumo mzima unatengeneza kazi za kuuza ndani ya nchi
Labels:
Michezo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment